Ajeruhiwa akihujumu miundombinu ya TANESCO

0
215

Mkazi mmoja wa mkoani Arusha, – Innocent Mòsha amejeruhiwa wakati akihujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Mòsha anadaiwa kukutwa na mkasa huo alipokuwa akiiba nyaya za shaba katika Transfoma, iliyopo katika kijiji cha Mandaka Mnono wilayani Moshi.

Akizungumzia tukio hilo, Afisa Uhusiano Huduma kwa wateja kutoka TANESCO mkoani Kilimanjaro, -Fredy Robert amesema kuwa, zaidi ya kaya 120 zimekosa umeme kutokana na hujuma hiyo.

Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Mandaka Mnono wanaoishi jirani na transfoma hiyo wamesema walisikia kelele za mlipuko katika tranfoma hiyo majira ya usiku, lakini hawakufuatilia zaidi kufahamu ni tukio gani.

Jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro limethibitsha kutokea kwa tukio hilo, na uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.