Ajali za barabarani zaongezeka

0
342

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema katika kipindi cha mwezi Julai mwaka 2021 hadi Machi mwaka huu ajali 1,594 zimeripotiwa kwenye vituo vya polisi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Amesema idadi hiyo ni tofauti na ajali 1,228 zilizoripotiwa kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Mhandisi Masauni ametoa takwimu hizo alipokuwa akiwasilisha bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Amesema takwimu zinaonesha kuwa ajali 366 za barabarani zimeongezeka ambazo ni sawa na asilimia 29.8.

Kati ya ajali hizo, 874 zilisababisha watu 1,191 kufariki dunia na 2,139 kujeruhiwa.

Mhandisi Masauni amesema ajali zimekuwa zikisababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na madereva kutozingatia sheria za usalama barabarani na ubovu wa magari,