Ajali yaua sita Tanga

0
150

Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya gari aina ya fuso yenye namba za usajili T 239 AFD walilokua wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika barabara ya Soni – Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Akizungumza na TBC kwa njia ya simu, Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi.

Kufuatia ajali hiyo, Kamanda Jongo amewataka watumiaji wa vyombo vya moto mkoani Tanga kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Lushoto na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.