Ajali yaua sita, 19 wajeruhiwa

0
268

Watu sita wamefariki dunia na wengine 19 wamejeruhiwa baada ya gari waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema, ajali hiyo imetokea eneo la Kwamdulu ambapo gari lililohusika katika ajali hiyo ni aina ya Coastal lenye namba za usajili T833 DMH.

Kamanda Jongo amesema miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe – Magunga na majeruhi wanaendelea kupata matibabu hospitalini hapo.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni mwendokasi wa gari hilo ambapo dereva alishindwa kulimudu na hivyo kushindwa kukata kona na kupinduka.

Kufuatia ajali hiyo, Kamanda Jongo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto mkoani Tanga kufuata sheria za usalama.barabarani ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.