Ajali yaua 9, wengine wajeruhiwa

0
216

Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace ambayo imekuwa ikifanya kazi ya kubeba magazeti iliyokuwa katika safari zake kuelekea mkoani Mbeya ikitokea Dar es Salaam.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo mkoani humo.

Kwa mujibu wa Kamanda Bukumbi, chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kugonga mti uliokuwa pembezoni mwa barabara na kupinduka, na hivyo kusababisha vifo vya watu tisa.

Amesema majeruhi watatu wa ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa.