Air Tanzania kuruka hadi Mumbai

0
351

Baada ya uzinduzi kuelekea Johannesburg mwezi uliopita, Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo Jumatano litazindua safari yake ya saba ya kimataifa kuelekea Mumbai nchini India.


Safari hiyo ya kwanza ya kuelekea Mumbai itafanyika saa moja na nusu jioni ya leo Julai 17 mwaka 2019, Safari tatu zitakuwa zikifanyika kwa wiki na nauli kwa sasa ni Dola za Kimarekani 378 sawa na Sh869,362 kwa tiketi ya kwenda na kurudi.