Afisa ardhi kikangoni

0
312

Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati ameliagiza jeshi la polisi mkoani humo kumkamata mara moja afisa ardhi wa wilaya ya Nzega, – Elisha Luponije kwa tuhuma za kujipatia fedha kutoka kwa Wananchi kinyume cha sheria.

Luponije anatuhumiwa kujipatia zaidi ya shilingi Laki Tisa kutoka kwa Idebe Luhaga na Fredy Kashinje ambao ni Wakazi wa kijiji cha Bukene wilayani Nzega kama malipo ya kodi ya ardhi, ujenzi na kubadilisha umiliki wa nyumba bila kuwapatia stakabadhi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Tuhuma hizo.ziliibuka wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Dkt. Sengati na kuwashirikisha baadhi ya Wakazi wa Bukene kwa lengo la kusikiliza kero za Wananchi na kuwahamasisha kuchukua vitambulisho vya Wajasiriamali.