ACT Wazalendo kuwasilisha utetezi wake kwa Msajili

0
405

Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, -Zitto Kabwe amesema kuwa chama hicho kitawasilisha utetezi wake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi ndani ya muda wa siku 14 waliopewa.

Zitto ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ikiwa ni siku moja tu baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini  kutishia kukifutia usajili chama hicho  kutokana na kukiuka sheria ya vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na kuchoma moto bendera ya Chama Cha Wananchi (CUF).

Katika barua yake  kwa ACT Wazalendo, Jaji Mutungi amekitaka chama hicho pia kuwasilisha maelezo ya maandishi,  kuwa ni kwanini usajili wake wa kudumu usifutwe kutokana na kutowasilisha ripoti ya ukaguzi kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2017.

Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amesisitiza kuwa chama hicho kinafanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi na hakijawahi kuvunja utaratibu.