Acheni kujichukulia sheria mkononi : IGP Sirro

0
235

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewaonya baadhi ya wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na hasa kufunga barabara kwa kuweka mawe na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine.

IGP Sirro ametoa onyo hilo akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha ambapo alilazimika kusimama katika kijiji cha Kelema wilaya ya Chemba mkoani Dodoma baada ya wananchi kufunga barabara kuu ya Dodoma – Babati kwa madai ya kuchoshwa na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika eneo hilo na kusababisha vifo na majeruhi.

Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamemuomba IGP Sirro kuwawekea askari wa kutosha wa usalama barabarani pamoja na kuweka matuta na beria, vitu vitakayosaidia kupunguza ajali.