Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema asilimia 37 ya bajeti ya Serikali inatoka katika mapato ya Bandari ya Dar es Salaam na kama atapatikana mwekezaji mahiri katika bandari hiyo takribani asilimia 67 ya bajeti ya Serikali itatoka katika bandari hiyo na itaisaidia katika kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuhusu uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.
“Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu. 37% ya bajeti ya Serikali inatoka bandari ya Dar es Salaam. Kama tutaweza kuwekeza vizuri na kupata mwekezaji mahiri takribani 67% ya mapato au bajeti ya Serikali itatoka kwenye bandari ya Dar es Salaam”. Amesema Profesa Mbarawa