15 mbaroni Dar kwa tuhuma za wizi

0
166

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa 15 kwa tuhuma mbalimbali za ujambazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne amesema watuhimiwa hao wamekamatwa katika maeneo tofauti wakiwa na vifaa mbalimbali vilivyoibwa ikiwemo nondo tani moja.

Vifaa vingine ni pamoja na pikipiki, gari aina ya Toyota Canter, kompyuta, laini za simu, magodoro pamoja na televisheni.

Kufuatia matukio hayo Kamanda Muliro amewaonya wahalifu wanaojihusisha na uhalifu wakutumia silaha za moto kuwa jeshi hilo liko imara kudhibiti uhalifu kwa njia yoyote ile kukomesha vitendo hivyo nchini.