102 wafutiwa matokeo form IV

0
309

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limewafutia matokeo watahiniwa 102 waliofanya udanganyifu wakati wa mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika mwezi Novemba mwaka 2023.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Said Mohammed amesema Wanafunzi watano waliandika matusi kwenye karatasi zao za kujibia mtihani.

Katika matokeo hayo jumla ya Watahiniwa 484,823 sawa na asilimia 87.65 ya Watahiniwa waliofanya mtihani huo wamefaulu.