Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amehukumiwa miezi kumi na tano jela na mahakama ya kikatiba ya nchi hiyo.
Hatua hiyo inafuata baada ya mahakama hiyo kumkuta na hatia ya kukaidi kufika mahakamani kutoa ushahidi juu ya tuhuma za rushwa wakati wa utawala wake.
Rais Jacob Zuma alimaliza utawala wake mwezi Februari 2018.