Zaidi ya nyumba laki tano zaharibiwa na mafuriko Sudan Kusini

0
329

Hali ya tahadhari imetangazwa katika eneo la Jonglei, Sudan Kusini kufuatia mafuriko yaliyolikumba eneo hilo.

Habari kutoka Sudan Kusini zinasema watu kadhaa wamebaki bila makazi huku nyumba zaidi ya laki 5 zikiharibiwa na mafuriko hayo.

Serikali ya Sudan Kusini imesema msaada wa kibinadamu unahitajika kwa haraka kwa ajili ya watu walioathiriwa na mafuriko hayo.