Yemen yaripoti kisa cha kwanza cha Corona

0
759

Wakati nchi zaidi ya 150 zikiwa zinalia kutokana na maafa ya homa ya Corona, nchi ya Yemen imethibitisha kuwepo kwa kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona leo Aprili 10.

Mapema leo hii, kamati kuu ya dharura ya kitaifa kwa ajili ya COVID-19 imemtangaza mgonjwa huyo kutoka Mkoa wa Hadhramout.

Mgonjwa huyo ni raia wa Yemen aliyekuwa akifanya kazi katika Bandari ya Ash Shihr.

Huku bandari hiyo ikifungwa, nchi hiyo ina wasiwasi mkubwa endapo ugonjwa huo utasambaa kwa kasi nchini humo, kwani hawana vifaa vya afya vya kutosha kupambana na janga hilo.