Xi Jinping : Muda wa kuionea China umekwisha

0
536


China inaendelea na maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo, ambacho kimeliongoza Taifa hilo kwa zaidi ya miaka 70.


Akilihutubia Taifa kwenye maadhimisho hayo katika uwanja wa Tiananmen mjini Beijing, Rais Xi Jinping wa China ameyaonya mataifa ya kigeni ambayo yamekuwa yakijaribu kuionea China, na kusema enzi za kufanya hivyo zimepitwa na wakati.


Amesema muda wa China kuburuzwa na kunyanyaswa na mataifa mengine kwa sasa haupo, na kwamba nchi hiyo imeidhihirishia dunia kuwa sio tu inaweza kuleta mabadiliko duniani, bali pia inaweza kuunda dunia mpya kwa maendeleo.


Xi ameahidi kuimarisha nguvu za kijeshi za Taifa hilo, kukirejesha kisiwa cha Taiwan chini ya himaya ya China pamoja na kuimarisha nafasi ya nchi hiyo katika uendeshaji wa mji wa Hong Kong.