William Ruto atangazwa Rais Kenya

0
166

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imemtangaza William Ruto kutoka muungano wa Kenya Kwanza kuwa mshindi wa kiti cha Urais kufuatia uchaguzi uliofanyika tarehe Tisa mwezi huu.

Ruto ametangazwa mshindi baada ya kupata asilimia 50.49 ya kura zote zilizopigwa.

Akitangaza matokeo hayo katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema mpinzani wa karibu wa Ruto, Raila Odinga kutoka muungano wa Azimio la Umoja yeye amepata asilimia 48. 08 ya kura zilizopigwa.

Wagombea wengine wa kiti hicho cha Urais nchini Kenya walikuwa ni George Wajackoyah na David Mwaure.

William Ruto anakuwa Rais wa tano kuliongoza Taifa la Kenya.