Mwigizaji Will Smith hatoruhusiwa kuhudhuria Tuzo za Oscar kwa miaka 10 kutoka sasa ikiwa ni adhabu baada ya kumpiga kibao Mchekeshaji Chris Rock jukwaani wakati wa Tuzo hizo za mwaka 2022.
Bodi ya Tuzo hizo imetangaza kwamba kwa miaka hiyo 10 kuanzia Aprili 8, 2022, Smith hatoruhusiwa kuhudhuria hafla au programu zozote za Academy, yeye binafsi au hata kwa mtandao.
Barua hiyo pia imeeleza shukrani nyingi kwa Chris Rock kwa utulivu wake wakati wa hali isiyo ya kawaida.
Baada ya marufuku hii ya miaka 10 Will Smith ameonesha kukubali adhabu aliyopewa kwa kuiambia CNN kwamba “ninakubali na kuheshimu uamuzi wa Academy”