Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa, virusi vya corona vinasababisha maafa makubwa kuliko hata mafua yenyewe yanayosababishwa na virusi hivyo, hivyo ni lazima dunia ichukue hadhari kubwa.
Shirika hilo limeshauri dunia nzima kushirikiana katika kutafuta suluhu ya virusi vya corona na kuyasaidia mataifa ambayo hayana uwezo wa kukabiliana na virusi hivyo.
WHO imeongeza kuwa licha ya corona kuanzia nchini China, lakini katika mataifa mengine ambako virusi hivyo vimesambaa maambukizi yamekuwa ya kasi, hali inayoendelea kuhatarisha usalama wa dunia.