WHO yasema huenda corona isitokomezwe kama ilivyo UKIMWI

0
381

Shirila la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa huenda ugonjwa hatari wa Corona, usitokomezwe kabisa duniani na ukabaki kuwa kama moja kati ya magonjwa hatari kama ilivyo UKIMWI.

WHO limetabiri kuwa njia pekee inayoweza kutokomeza Corona dunia ni pamoja na kuwapatia watu chanjo dhidi ya ugonjwa huo, kwani umekuwa na tabia ya kujirudia, kwa watu ambao tayari wameugua na kupona.

Corona pia imekuwa na tabia ya kulipuka tena katika maeneo ambayo awali ulisababisha maafa na kutokomezwa.