Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani afariki.

0
253

Pole zimekuwa zikitolewa kufuatia kifo cha Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Colin Powell ambaye amefariki dunia mwili kuudhoofishwa na UVIKO-19.

Kiongozi huyo wa zamani wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani alifariki dunia Oktoba 18, 2021.

Powell alikuwa ni Mmarekani Mweusi wa kwanza Kuwa waziri wa mambo ya nje mwaka 2001 chini ya utawala wa George W. Bush.

“Tumempoteza baba, babu, msimamizi wa familia na Mmarekani aliyetumikia Taifa lake” imesema familia yake katika taarifa maalum ya kutoa shukrani kwa wafanyakazi wa kituo Cha afya Cha Walter Reed kwa kutoa huduma nzuri kwake.

Powell alikuwa alipata ugonjwa wa Kansa ya damu ambayo ilimuweka katika hali mbaya baada ya kuanza kupata dalili za kuambukizwa UVIKO-19.