Waziri Mkuu wa Sudan anusurika kuuawa

0
498

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok amenusurika kifo kufuatia jaribio la mauaji lililotekelezwa mapema leo asubuhi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Taarifa kutoka shirika la habari la Taifa hilo imeeleza kuwa Hamdok amepelekwa kwenye eneo salama baada ya mlipuko huo uliolenga msafara wake.

“Msafara wa waziri mkuu umeshambuliwa wakati akielekea ofisini kwake lakini yupo salama,” taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu imeeleza.

Bado wahusika wa shambulio hilo hawajafahamika, lakini kundi la al Shabaab limekuwa likipambana kuing’oa serikali inayotambuliwa kimataifa ili kuweka dola ya Kiislamu inayofuata Sharia.

Hamdok aliteuliwa Waziri Mkuu wa Sudan Agosti 21, 2019.