Waziri Mkuu wa Ivory afariki dunia

0
183

 
Waziri Mkuu wa Ivory Coast, – Hamed Bakayoko amefariki dunia katika hospitali moja nchini Ujerumani.

Bakayoko ambaye alikuwa akitibiwa maradhi ya saratani hospitalini hapo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 56.

Mwezi Julai mwaka 2020, Bakayoko aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Ivory Coast kufuatia kifo cha ghafla cha Amadou Gon Coulibaly ambaye alikuwa akishikilia wadhifa huo.

Bakayoko alisafirishwa kwenda nchini Ufaransa mwezi Februari mwaka huu kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini baadaye alihamishiwa nchini Ujerumani baada ya afya yake kuendelea kuzorota.

Katika salamu zake za pole kufuatia msiba huo, Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast amemuelezea Bakayoko kuwa alikuwa kiongozi mwenye  mapenzi na nchi yake.