Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan ambaye anakabiliwa na shinikizo la kumtaka ajiuzulu amesema, hatafanya hivyo licha ya wapinzani wake kupanga kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Licha ya kukabiliwa na shinikizo hilo kutoka kwa wabunge wa upinzani, Khan pia anakabiliwa na upinzani kutoka ndani ya chama chake ambapo Wabunge 20 kutoka chama hicho wamejiunga na upinzani kumshikiniza ajiuzulu.
Tayari chama mshirika ambacho kilishiriki kuunda Serikali ya Pakistan kimejiondoa katika ushirika huo na kufanya upinzani kuwa na Wabunge wengi bungeni.
Kutokana na hatua hiyo upinzani unakuwa na Wabunge 172 kati ya Wabunge 342 wa bunge la Pakistan.