Watatu wagundulika kuwa na Omicron

0
189

Kenya imegundua visa vitatu vya kwanza vya aina mpya ya virusi vya Covid 19 , Omicron vilivyogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini mwezi uliopita.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema visa hivyo vimegunduliwa miongoni mwa wasafiri.

Wiki iliyopita, Uganda ilitangaza kuwa imegundua visa vya Omicron kwa wasafiri wanaokwenda nchini humo.

Visa hivyo vimegunduliwa kwa watu waliopimwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe ambao walisafiri kwa ndege kutoka nchi tano tofauti, mamlaka ya matibabu ya Uganda ilisema katika taarifa.

Watano wametoka wametoka Nigeria, wawili kutoka Afrika Kusini – ambapo aina hiyo iliripotiwa mara ya kwanza – na wawili kutoka Falme za Kiarabu.