Washukiwa mauaji ya AKA wakamatwa

0
302


Watu watatu wamekamatwa jijini Cape Town kwa mauaji ya rapa wa Afrika Kusini, Keinan Forbes (AKA) aliyeuawa kwa kupigwa risasi jijini Durban Februari 10, 2023.

Washukiwa hao wamekamatwa baada ya polisi kuwafuatilia kwa ukaribu kwa takribani wiki moja.

CApe Town ETC imeripoti kuwa, washukiwa hao watapelekwa Durban kesi hiyo itakaposikilizwa.

Moja ya walinzi wa marehemu AKA walisema katika mahojiano kuwa ulinzi wa rapa huyo kwa siku hiyo haukuwa imara kama ilivyozoeleka na yeye angeshauri AKA asiende katika mgahawa ule.