Wasaidizi wa Borris wajiuzulu.

0
244

Wasaidizi wanne wa ngazi ya juu wa Waziri Mkuu was Uingereza, Borris Johnson wamejiuzulu kwa muda mfupi kufuatia shinikizo la shutuma zinazomkabili waziri mkuu huyo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Jack Doyle amethibitisha kuondoka kwake muda mfupi baada ya kuondoka kwa kiongozi wa sera Munira Mirza.

Siku ya Alhamis kiongozi wa wafanyakazi katika ofisi hiyo Dan Rosenfield na mtumishi mwingine wa ngazi ya juu, Martin Reynolds nao walifuatia kuondoka.

Kujiuzulu kwa viongozi hao wa ngazi ya juu kunakuja kufuatia Borris kubanwa na maswali mengi kuhusu uongozi wake ndani ya chama.

Tamko kutoka kwa msemaji wa ofisi ya waziri mkuu limesema Rosenfield alitoa barua yake ya kujiuzulu kwa waziri mkuu mapema siku ya Alhamis ila atabaki mpaka mrithi wake atakapopatikana.

Kiongozi msaidizi wa chama cha Labour, Angela Rayner amesema wakati wasaidizi wa ngazi ya juu wa Borris wakiacha kazi, pengine ni muda wa yeye [Borris] kujitazama na kufikiria tatizo ni nini.