Mke wa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi,
Mama Mariam Mwinyi, amewasihi Wanawake wa Kitanzania wanaoishi nchini Qatar (Diaspora) kuendelea na utaratibu wa kuchangia maendeleo nchini mwao.
Mariam Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora ameyasema hayo Doha, Qatar
alipokuwa akizungumza na Diaspora Wanawake walioko nchini humo.
Pia amewasisitiza Wanawake wa Kitanzania hasa Diaspora wanaoishi Qatar kuwa makini katika malezi ya watoto, kufuatia kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji.
Amesema ni muhimu kwa akina Mama kuwa mstari wa mbele katika kuzuia vitendo vya udhalilishaji na pia amewasihi wahakikishe watoto wanapata malezi bora.