Wananchi wahamasishwa kulinda Mji Mkuu Addis Ababa

0
298

Maofisa katika Mji Mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa wamewataka wakazi kusajili silaha zao na kuwa tayari kulinda maeneo yao kufuatia wasiwasi wa waasi kuuvamia mji huo.

Ombi hilo limekuja siku kadhaa baada ya kundi la Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kusema kwamba wamekamata miji miwili kilomita 400 kutoka mji mkuu Addis Ababa.

Serikali kuu imetangaza hali ya tahadhari nchini kote

Marekani imewasihi waasi hao kutokujaribu kuuvamia na kuuteka mji huo mkuu wenye watu zaidi ya milioni tano.

Mapambano hayo yalianza mwaka mmoja uliopita katika sehemu ya Kaskazini mwa nchi hiyo ambapo kundi hilo la lilivamia na kuteka miji ya jirani kama Amhara na Afar.