Wananchi wa Uingereza kurejea kazini

0
384

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa maelezo ya  kurejesha hali ya kawaida nchini humo baada ya awamu ya kwanza ya kudhibiti wananchi kutoka nje ili kudhibiti maambukizi ya Corona.

Akihutubia taifa hilo kwa njia ya runinga, Johnson amesema kuanzia Jumatano wakazi wa England wataruhisiwa kufanya shughuli zao nje kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya janga hili.

Aidha, waziri mkuu huyo amesema, wafanyakazi wa viwandani wanapaswa kurejea katika maeneo yao ya kazi, lakini waepuke usafiri wa umma.

Johnson amewataka wananchi kuchukua taadhari za kujikinga na maambukizi ya viruzi vya Corona wakati wote.