Wananchi: Polisi wanatusumbua sana

0
411

Baadhi ya Wananchi wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamelalamikia namna ambavyo wanapata shida wanapokuwa na mashtaka na kupelekwa katika vituo vya polisi.

Angelo Gabriel, mkazi wa Mlele amesema, kumekuwa na usumbufu mkubwa na wakati mwingine wanapewa kesi ambazo sio za kweli na pia hulazimika kutoa rushwa ili waachiwe huru.

Angelo amewaambia wajumbe wa Tume ya Rais ya Haki Jinai kuwa mara kadhaa Wananchi wamekamatwa na nyama pori ambazo wameuziwa na wahusika lakini baada ya muda wanakamatwa na kulipishwa pesa.