Wananchi Bolivia wapinga kuendelea kuzuiwa kutoka nje

0
422

Polisi nchini Bolivia wapambana ili kutuliza ghasia za waandamanaji wanaopinga hatua ya serikali ya nchi yao kuendelea kuwazuia kutoka nje ya makazi yao kwa hofu ya Corona.

Waandamanaji hao wamesema wamechoka kukaa ndani huku serikali ya nchi hiyo ikishindwa kuwapatia mahitaji muhimu kwa ajili ya familia zao ikiwemo chakula.

Wanasema muda wa kukaa ndani umetosha hivyo ni vema wakatoka kujitafutia mahitaji, kwani serikali haijui ni kutu gani wanahitaji na haijui ukubwa wa familia zao.