Wanajeshi kuhifadhi mbegu za uzazi

0
286

Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa ripoti zinazoeleza wanajeshi wa Urusi walioitwa vitani Ukraine kupata fursa ya huduma isiyo na malipo ya kuhifadhi mbegu za kiume kwa njia ya kuzigandisha, ili zitumike baadaye zitakapohitajika.

Kwa nchi zilizoendelea utaratibu huo unaonekana kuwa wa kawaida hasa kwa wanajeshi, ambao hutamani kuwa na uwezo wa kuendeleza kizazi chao hata baada ya kushindwa kurejea nyumbani.

Kwa kujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Urusi Igor Trunov, mwezi Desemba mwaka 2022 wanajeshi wa nchi hiyo waliotakiwa kwenda kupigana vita nchini Ukraine walipewa fursa ya kuhifadhi bila malipo mbegu zilizogandishwa kwenye benki inayofahamika kama cryobank.

Ripoti zinaeleza kuwa Urusi ilikusanya wanajeshi wa akiba laki tatu wa kupatiwa huduma hiyo na baadaye
wanaume wengine waliendelea kujiorodhesha ili kuipata.

Mataifa kama Uingereza wanatumia njia hiyo ya kuhifadhi mbegu za kiume kwa njia ya kuzigandisha
ili kuhakikisha wanajeshi wao wanaweza kuwa na uzazi pale wanapohitaji.