Wanajeshi El Salvador wavamia bunge

0
436

Wanajeshi na maafisa wa polisi nchini El Salvador wamevamia bunge la nchi hiyo na kushinikiza kuidhinishwa kwa mkopo wa dola milioni 109 za Kimarekani (TSh bilioni 252) ili kuwanunulia vifaa vyenye ubora vya kukabiliana na matukio ya uhalifu.

Wanajeshi hao waliingia katika jengo la bunge wakati Rais wa nchi hiyo, Nayib Bukele akijiandaa kuhutubia Bunge.

El Salvador ina kiwango cha juu cha mauaji duniani, ambapo watu 95 hufa kila siku katika mauaji yanayohusisha vitendo vya uhalifu.