Waliofariki baada ya jengo kuporomoka Lagos wafikia 15

0
318

Kikosi cha uokoaji Lagos, Nigeria kinaendelea na jitihada za kutafuta watu walionaswa kwenye jengo la ghorofa 22 lililoporomoka Jumatatu Novemba 1, 2021 na hadi sasa idadi ya waliofariki imeongezeka kutoka sita hadi kufikia 15.

Inasemwa kuwa kulikuwa na watu zaidi ya 100 ndani ya jengo hilo ambalo bado lilikuwa linajengwa.

Hadi sasa bado timu hiyo ya uokoaji inaendelea na kuwatafuta watu wengine ambao bado hawajapatikana