Waendesha mashtaka nchini Marekani wamesema watu 70 wameshtakiwa kwa makosa ya uhalifu, baada ya kushiriki kwenye ghasia huko Capitol Hill wiki iliyopita na kusababisha fujo katika bunge la Congress.
Fujo hizo zilisababisha mauaji na baadhi ya watu kujeruhiwa, huku pia kukitokea uharibifu wa mali za bunge.
Watu hao walihamasishwa kufanya fujo na Rais Donald Trump wa nchi hiyo aliyekuwa akipinga matokeo ya uchaguzi wa Rais nchini humo.
Trump aliwahamasisha wafuasi wake kwenda bungeni kuwazuia Wabunge kupiga kura ya kumthibitisha mpinzani wake Joe Biden.
Rais Trump mwenyewe amesema kuwa hotuba yake aliyoitoa wiki iliyopita alipowataka wafuasi wake kuvamia bunge la Congress ilikuwa sahihi.
Trump ataachia wadhifa wake wa Urais tarehe 20 mwezi huu, siku ambayo Joe Biden ataapishwa.