Waigizaji filamu waliopiga pesa ndefu 2023

0
350

Chapisho la Forbes limetoa orodha ya waigizaji 10 wa filamu walioingiza kipato kikubwa zaidi kwa mwaka 2023.

Kwa mujibu wa chapisho hilo, Mwigizaji wa Filamu na Raia wa Marekani, Adam Sandler mafanikio yake katika tasnia ya burudani aliongoza orodha ya waigizaji waliolipwa fedha nyingi zaidi kwa kuingiza mapato ya takribani dola za Marekani milioni 73.

Margot Robbie, Raia wa Australia ambaye ni mtozi wa filamu pamoja na Tom Cruise vipato vyao vimekaribiana na kuwafanya kushika nafasi ya pili na ya tatu kwa kuingiza mapato ya dola milioni 59 na 45 mtawalia.

Wengine na vipato vyao vya dola kwenye mabano ni Ryan Gosling (milioni 43), Matt Damon (milioni 43), Jennifer Aniston (milioni 42), Leonardo Dicaprio (milioni 42), Jason Statham (milioni 42), Ben Affleck (milioni 38) na Denzel Washington dola milioni 24.