Virusi ya Corona vyazidi kusambaa Duniani

0
473

Serikali ya China imeweka karantini katika jimbo la Wuhan, kulikozuka ugonjwa unaosababishwa na virusi hatari vya Corona vinavyoweza kusababisha maafa baada ya watu tisa nchini humo kufa kutokana na virusi hivyo.

Watu wengine zaidi ya sitini wameambukizwa virusi vya Corona, nchini humo, huku virusi hivyo vikiendelea kusambaa katika nchi nyingine, hali ambayo inaashiria kuwa vinaweza kuambukizwa kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu mwingine.

Virusi vya Corona vinaambukizwa kutokana na wanyama, lakini habari zinasema, tayari mgonjwa mwingine wa virusi hivyo amebainika nchini Marekani, huku tayari virusi hivyo vikiwa vimeingia katika nchi ya Thailand.

Virusi hivyo pia vimeingia nchini Japan na wiki hii mgonjwa mmoja wa virusi vya Corona alibainika kuwa ameambukizwa nchini Korea Kusini, ambaye alikuwa amewasili nchini humo akitokea China.