Vijiji vyashambuliwa, watu 26 wauawa

0
272

Watu wenye silaha wameshambulia vijiji vinne katika jimbo la Plateau nchini Nigeria na kuua watu 26.

Vijiji hivyo ni Gyambau, Kyaram, Dungur na Kukawa.

Habari kutoka nchini Nigeria zinaeleza kuwa watu hao waliokuwa na silaha wakiwa kwenye pikipiki, wamevishambulia vijiji hivyo na kuanza kurusha risasi hovyo na hivyo kusababisha vifo.

Wengi wa waliofariki dunia katika tukio hilo ni watoto.

Watu hao pia wamefanya uharibifu mkubwa katika vijiji hivyo ikiwa ni pamoja na kuchoma moto nyumba na kuiba ngombe.

Polisi katika jimbo la Plateua wanasema idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwa kuwa wakazi wengi wa vijiji hivyo hawajulikani walipo na inadhaniwa kuwa wameuawa,

Shambulio hilo limesababsha wakazi wengi kuyahama makazi yao.