Video ya ‘Baby Shark’ yavunja rekodi ya YouTube kwa video ya kwanza kufikisha watazamaji bilioni 10
Video hiyo imeeandaliwa na Kampuni ya Pinkfong na awali iliimbwa na mwimbaji Hope Segoine mwenye umri wa miaka 10 mwaka wa 2015, “Baby Shark” ilipandishwa(Uploaded) kwenye mtandao wa YouTube Juni 2016.
Tangu kuachiliwa kwake, wimbo umewavutia watoto zaidi na watu wazima, ukichochewa na michezo mbalimabali na kusambaa katika mitandao ya jamii huku waimbaji na watu mashuhuri kwa kasi wameupa wimbo huo nguvu.
Kwa mfululizo wa wiki 20 wimbo huo umeshika chati kwenye Billboard Hot 100 pamoja na kuidhinishwa na RIAA Diamond (11x Platinum).
Kampuni iliyoandaa wimbo huo pia ilitoa mfululizo wa uhuishaji wa shule za awali pamoja na Nickelodeon Animation Studio inayoitwa Baby Shark’s Big Show!, iliyoonyeshwa kwa mara ya kwanza mwaka 2021 na imefikia watazamaji zaidi ya milioni 26 katika channel ya Nickelodeon na Nick Jr.