Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa maambukizi ya UVIKO -19 sio tena janga la dunia.
Tangazo hilo la WHO linatoa mwelekeo.mzuri wa kumalizika kwa janga hilo na limekuja miaka mitatu baada ya kutangazwa kwa kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa huo.
Taarifa za WHO zinaonyesha kupungua kwa idadi ya vifo duniani kote kutokana na UVIKO -19, ambapo vimepungua kutoka zaidi ya watu laki moja kwa wiki mwezi.Januari mwaka 2021 hadi kufikia zaidi ya watu 3,500 Aprili 24, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, takribani watu Milioni saba wamefariki dunia katika janga hilo.la UVIKO – 19 duniani kote.
Hata hivyo amesema idadi sahihi inaweza kukaribia vifo Milioni 20 na kuonya kuwa UVIKO bado ni tishio hivyo muhimu watu kuendelea kuchukua tahadhari.