Utata waendelea kuhusu Khashogi

0
1351

Habari kutoka nchini Uturuki zinasema kuwa Mwandishi wa habari na mtu ambaye amekuwa akiikosoa serikali ya Saudi Arabia, -Jamaal Khashogi bado yuko ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia ulioko mjini Istanbul.

Awali gazeti moja la nchini MAREKANI lilitangaza kuwa mwandishi huyo wa habari amepotea katika mazingira ya kutatanisha na mara ya mwisho alionekana akiingia katika ubalozi huo mdogo wa Saudi Arabia.

Rafiki wa kike wa Khashogi amesema kuwa rafiki yake alikwenda kwenye ubalozi huo kuchukua nyaraka muhimu ambazo zingemsaidia katika kazi yake, lakini matokeo yake hakurejea nyumbani.

Tukio hilo lilisababisha afisa mmoja wa serikali ya Uturuki kutangaza kuwa mwandishi huyo bado yuko kwenye ubalozi huo, lakini kumekuwa na wasiwasi kuhusiana na usalama wake kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akiukosoa utawala wa Saudi Arabia na mfalme wa nchi hiyo.