Urusi yatenga siku ya kupata ujauzito

0
438

Katika hotuba yake ya hali ya uchumi ya mwaka 2006, Rais Vladimir Putin wa Urusi alitaja idadi ndogo ya watu kuwa ni tatizo kwa mustakabali wa Taifa hilo.

Na ndipo akatangaza jitihada za kuongeza kiwango cha idadi ya watu nchini Urusi, ikiwa ni pamoja na kutoa motisha ya pesa taslimu kwa familia ambazo zina mtoto mmoja ili zihamasike kuongeza watoto.

Septemba 12 kila mwaka ni siku muhimu sana nchini Urusi hasa eneo la Ulyanovsk, ambapo wanaipa heshima kama siku ya kupeana ujauzito kwa raia wa Urusi.

Utamaduni huo kawaida unazungumzia wenza kupata muda maalum wa faragha ya ndoa na uzazi.

Hivyo, serikali ya Urusi ikaanzisha siku ya mapumziko kwa umma maalumu kwa ajili ya kuwapa wanandoa muda wa faragha kwa matumaini kwamba watashika mimba. Wazazi ambao watoto wao huzaliwa miezi tisa baadaye wanaweza hata kushinda zawadi kwa kusaidia kuwa mstari wa damu kuendelea damu ya Urusi. Watoto wanaozaliwa Septemba 12 hupata zawadi kutoka kwa Mamlaka.

Mnamo mwaka 2005, Gavana Sergey Ivanovich Morozov wa Ulyanovsk, eneo lililoko kilomita 800 Mashariki mwa Moscow, aliongeza kipengele cha kufurahisha kwa kampeni ya kitaifa kwa kutangaza Septemba 12 kama Siku ya kupeana ujauzito na kuwapa wanandoa likizo ya kazi ili kupata fursa ya faragha kwa ajili ya kutengeneza kizazi kijacho.

Tuzo kuu ya 2007 ilikwenda kwa Irina na Andrei Kartuzov, ambao walipokea UAZ-Patriot, gari la kifahari huko Ulyanovsk.

Washiriki wengine walizawadiwa kamera za video, TV, friji na mashine za kufulia.

Urusi imeamua kutenga siku hiyo na zawadi zingine kama hamasa kutokana na viwango vya uzazi nchini humo kupungua pamoja uwiano usio sawa kati ya wanaume na wanawake na maisha mafupi ya wanaume wa Urusi yanaleta wasiwasi mkubwa kwa jamii.