Upepo Mkali wasababisha vifo

0
503

Watu sita wamekufa, wote wakiwa ni watalii, na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya upepo mkali unaoambatana na tufani kuikumba nchi ya Ugiriki, hasa katika eneo ambalo watalii wengi hupenda kutembelea.


Serikali ya nchi hiyo imetangaza hali ya tahadhari baada ya tufani hiyo kuupiga mkoa wa Halkidiki, ulioko karibu na mji wa Pesaloniki ambao ni maarufu kwa masuala ya utalii.


Upepo huo ambao pia ulikuwa ukiambatana na mvua za msimu, umeng’oa miti mikubwa na kupindua magari yaliyokuwa yakipita barabarani na mengine yaliyokuwa yameegeshwa