Mchakato wa kumchagua waziri mkuu mpya wa Uingereza unaendelea, ambapo chama tawala cha Conservative kinaendelea kuwachuja wagombea, kuziba nafasi iliyoachwa wazi baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Boris Johnson.
Waziri wa zamani wa fedha Rishi Sunak anaongoza katika kinyang’anyiro hicho kinachohusisha wagombea wanne
wakiwemo wanawake watatu.
Miongoni mwa wagombea hao watatu wanawake mmoja ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Afrika.
Awali kamati ya uchaguzi ya chama cha Conservative ilimuengua mgombea Tom Tugendhat ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya chama na mkosoaji mkubwa wa Boris Johnson .