Uingereza yalia na joto kali

0
200

Wizara ya Afya nchini Uingereza imetangaza mpango wa dharula wa kuhudumia wagonjwa wanaougua kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha joto nchini humo.

Kaimu Waziri Mkuu wa nchi hiyo Dominic Raab amesema, maafisa wa afya nchini humo wametenga vituo maalum vya kupokea wagonjwa walioathirika kufuatia kuongezeka kwa kiwango cha joto.

Wataalam wa hali ya hewa nchini Uingereza wamesema, kwa siku ya leo joto katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo lilitarajiwa kuwa nyuzi joto 41.

Kiwango cha joto kimeongezeka nchini Uingereza huku matukio ya moto kuteketeza misitu yakiendelea katika maeneo kadhaa barani Ulaya ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Ugiriki, Hispania na Kaskazini mwa Morocco Barani Afrika

Zaidi ya watu elfu 14 wamehamishwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa ambapo vikosi mbalimbali vya zimamoto vinaendelea kuzima moto unaoendelea kuwaka barani Ulaya