Uingereza Yaendelea Kuzuia Meli ya Mafuta ya Iran

0
351

Wizara ya ulinzi nchini Uingereza imetangaza nia yake ya kuendelea kuzuia meli ya mafuta ya Iran ambayo imefika katika eneo la Gigraltar, meli inayojulikana kama Grace One.

Meli hiyo ya Iran ilizuiliwa na meli za kijeshi za nchi ya Uingereza mwezi uliopita, kwa madai kuwa nchi hiyo imekuwa ikikiuka vikwazo vya kimataifa ambavyo nchi ya Syria imewekewa kuhusiana na mafuta.

Meli hiyo ilikuwa njiani kupeleka mafuta nchini Syria, nchi ambayo bado inakabiliwa na mapigano. Mahakama nchini Uingereza imeamuru kuwa serikali ya nchi hiyo itaendelea kuishikilia meli hiyo ya Iran baada ya kukiuka vikwazo vya kimataifa.

Jana meli za kijeshi nchi za Marekani na Uingereza zilionekana zikifanya doria katika eneo la Ghuba na rais wa Iran akashutumu hatua hiyo na kusema kuwa nchi za Ghuba zina uwezo wa kujilinda bila kuhitaji msaada kutoka katika mataifa ya kigeni.