Uingereza kuwapa uraia wakazi wa Jimbo la Hong Kong

0
704

Waziri Mkuu wa Uingereza, Borris Johnson amesema nchi yake iko tayari kuwapatia uraia mamia ya wakazi wa Jimbo la Hong Kong nchini China endapo nchi hiyo itendelea kupitisha miswada inayowakandamiza wakazi wa kisiwa hicho.

Hivi karibuni China imepitisha muswada unaohusiana na wimbo wa taifa wa nchi hiyo jambo lililosababisha maandamano makubwa katika kisiwa cha Hong Kong huku watu zaidi ya 300 wakitiwa mbaroni kwa kuhusika na maandamano hayo.