Uhuru rasmi kumuunga mkono Raila

0
352

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza rasmi kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuchukua nafasi ya urais baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9.

Rais Kenyatta amewataka wanaomuunga mkono kuungana na Odinga katika uchaguzi huu na kusema Kuwa kiongozi huyo analipenda taifa lake kutoka moyoni.

Amesema Odinga anajua nchi inaelekea wapi, kwa hiyo atahisi amani kumuachia nchi.

Hii itakuwa mara ya tano kwa Odinga kugombea urais na inaaminika kwamba itakuwa mara yake ya mwisho

Kufuatia tamko hilo la Rais Kenyatta, Naibu Rais wa sasa wa taifa hilo William Ruto anaonekana kuwekwa kando ingawa pia ametangaza kugombea urais kupitia muungano wa United Democratic Alliance