Uhaba wa mafuta waendelea kuitesa Sri Lanka

0
167

Shule nchini Sri Lanka zimefungwa kwa muda wa wiki ya tatu mfululizo, kutokana na uhaba wa mafuta ya kuendeshea magari ya kusafirisha walimu na wanafunzi.

Waziri wa Elimu nchini humo Nihal Ranasinghe amewataka walimu na wanafunzi ambao wameathirika na tatizo hilo kutumia mafunzo kwa njia ya mtandao hadi pale tatizo hilo litakapokuwa limepatiwa ufumbuzi.

Waziri wa Nishati wa Sri Lanka, Kanchana Wijesekera amesema, shehena ya kwanza ya mafuta ya tani elfu 40 inatarajiwa kuwasili nchini humo tarehe 22 mwezi huu.

Serikali ya Sri Lanka inahitaji dola milioni 587 kwa ajili ya kununulia mafuta ambapo nchi hiyo inadaiwa dola milioni 800 na wasambazaji wa mafuta kutokana na deni la kuagiza nishati hiyo nchini humo.